Friday, May 24

Trump asema mpango mpya wa uhamiaji Marekani kuzingatia elimu, ujuzi

0Pendekezo la Trump ni kuwa Marekani itaendelea kutoa green cards au ukazi wa kudumu kwa watu milioni 1.1 kila mwaka, lakini itabadilisha jinsi watakavyo chaguliwa.

Ameeleza kuwa mfumo huo utatoa kipaumbele kwa wale wenye ujuzi wa hali juu na wengine walio na elimu ambayo ina wawezesha kuajiriwa katika nafasi ambazo kunaupungufu wa wataalam na fursa za uwekezaji, badala ya mafungamano ya kifamilia na raia wa Marekani na mahitaji ya kibinadamu.

Trump ameongea hayo Alhamisi White House katika bustani ya Rose Garden, akisisitiza kuwa nchi nyingine kama vile Canada zimekuwa zikitekeleza utaratibu huo kwa kutumia vigezo vya elimu na ujuzi kwa miaka mingi.

Hivi sasa, asilimia 12 ya wahamiaji wanapewa ruhsa kuingia nchini Marekani kwa sababu ya ujuzi waliokuwa nao, na asilimia 66 ni kwa sababu ya mafungamano yao ya kifamilia ya wale ambao tayari wako kisheria nchini.

Chini ya mpango huu, asilimia 57 ya visa za uhamiaji zitatolewa kwa wale wenye ujuzi fulani au nafasi za kazi, na asilimia 33 tu zitakwenda kwa watu wenye mafungamano ya kifamilia. Visa ambazo zinatolewa kwa ajili ya mahitaji ya kibinadamu zitapunguzwa kutoka asilimia 22 kufikia asilimia 10.

Sababu za kiuchumi za kuondoa au kupunguza kwa kiasi kikubwa nafasi za uhamiaji kutokana na mafungamano ya kifamilia linadadisiwa na wachambuzi wa masuala ya uhamiaji.

David Bier wa Tasisi ya kidemokrasia CATO amesema takriban nusu ya wahamiaji wanaodhaminiwa na familia wana shahada za vyuo vikuu, ambao ni idadi kubwa kuliko ya watu waliozaliwa Marekani.

Share.

Leave A Reply