Saturday, August 24

Mueller asema hakupewa muongozo wa kumshtaki Trump

0Amesema hayo wakati akitangaza kufungwa kwa ofisi yake baada ya kuhitimisha mwisho wa mwezi Machi uchunguzi uliochukuwa miezi 22 juu ya Russia kuingilia kati uchaguzi wa urais wa Marekani 2016 na uwezekano kwamba Trump alizuia sheria isifuate mkondo wake.

Akieleza maoni ya kisheria ya muda mrefu ya Idara ya Sheria kuwa rais aliyeko madarakani hawezi kushtakiwa, Mueller aliwaambia waandishi katika maelezo yake ya kwanza kwa umma : “Kumshtaki Rais kwa kosa la jinai, hivyo, siyo kitu ambacho tungeweza hata kufikiria.”

Amesema kuwa itakuwa sio “haki kuweza kumtuhumu mtu kwa kosa wakati hakuna azimio la mahakama kwa shtaka linalohusika.”

Lakini, aliongeza kuwa “Ingekuwa tunauhakika kuwa rais hakutenda kosa la jinai, tungesema hilo.”

Mwendesha mashtaka maalum ametangaza kuwa anajiuzulu kutoka Idara ya Sheria akirejea uraiani kuishi maisha yake binafsi.

Alikuwa ni mshirika wa Kampuni ya mawakili ya WilmerHale, Washington, D.C kabla ya kuchaguliwa kuwa mwendesha mashtaka maalum kuichunguza Russia Mei 2017.

Mueller alikuwa amehitimisha Ripoti ya siri yenye kurasa 448 juu ya uchunguzi huo aliyoituma kwa Mwanasheria Mkuu William Barr akieleza kwamba hakuna ushahidi kwamba kampeni ya Rais Trump ilishirikiana na Moscow katika vitendo vya uhalifu.

Lakini suala iwapo Trumpalizuia uchunguzi usifanyike, mwendesha mashtaka maalum amesema kwa kuwa asingeweza kupendekeza kufunguliwa mashtaka ya kidesturi dhidi ya Trump, pia hakuweza kumsafisha kuwa hana makosa, akieleza matukio 11 ambayo yanaweza kuwa ni vitendo vya kuzuia sheria kuchukua mkondo wake.

Share.

Leave A Reply