Monday, August 26

STAND UNITED WAISHANGAA TFF…SASA WAPIGA DEBE KUSAKA WACHAWI WA SHERIA ZA SOKA

0
Uongozi wa klabu ya wapiga Debe wa Stand united maarufu Chama la wana ya mjini Shinyanga, umesema haujaridhishwa na maamuzi ya shirikisho la soka nchini, TFF, la kuishusha daraja klabu hiyo inayolingana alama na timu ya Kagera Sugar ambayo imebakizwa ligi kuu soka ya Tanzania bara, licha ya Stand United kuongoza kwa magori mengi ya kufunga.

 Mwenyekiti wa Stand United Chama la wana Dk. Ellyson Maeja, amesema wameshangazwa na maamuzi ya TFF ya kuishusha daraja Stand United mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu soka ya Tanzania bara, kwa vigezo vya magoli ya kufungwa licha ya kuongoza kwa magoli ya kufunga dhidi ya timu ya Kagera Sugar ambayo inalingana alama 44 katika msimamo wa ligi hiyo.

Stand United hadi ligi kuu inamalizika imeshinda mechi 12 na kufungwa mechi 18 magoli ya kufunga magoli 38 na kufungwa 50 huku Kagera Sugar ikishinda mechi 10 na kufungwa mechi 14 imefunga magori 33 na kufungwa magori 43.

Kufuatia hali hiyo ambayo imeleta mijadala mbalimbali kwa mashabiki wa soka na klabu ya Stand United uongozi umepanga kutafuta washauri na wabobezi wa sheria za soka ambapo klabu hiyo itatoa tamko rasmi la kukubali kushuka daraja au kukata rufaa.

Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

Leave A Reply