Saturday, August 24

Waziri Lugola atoa agizo Mkuu wa polisi Geita kusimamishwa kazi

0


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwasimasha kazi mkuu wa polisi Geita, mpelezi wa wilaya na mkuu wa kituo cha polisi Geita kupisha uchunguzi kufuatia tukio la kutoroka mahabusu 15 Mei 21 mwaka huu.

Pia ameagiza askari wengine nane waliokuwa wakiwalinda mahabusu hao kuwekwa ndani.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia tukio la mahabusu 15 kutoroka mapema wiki hii Mei 24 wakiwa kwenye jengo la Mahakama ya Mkoa wa Geita walipofikishwa kwaajili kusikiliza kesi zao.


Share.

Leave A Reply