Wednesday, August 21

Wananchi wahimizwa kulipia huduma ya maji

0
Na Amiri kilagalila.

Wakati Serikali inayo jukumu la kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi, salama na yenye kutosheleza, wananchi nao wanapaswa kutimiza wajibu kwa kulipia huduma hiyo kadri wanavyotumia maji kama walivyokubaliana na mamlaka zinazotoa huduma katika maeneo yao.

Naibu Waziri wa Maji Mh.Juma Aweso (mb) amesema hayo wakati akizindua jengo la mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Geita (GEWASA) lililopo katika kata ya kalangalala mjini Geita.

“Bei ya maji huidhinishwa na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Ewura, baada ya utaratibu maalum kufanyika ikiwamo kuwashirikisha wadau wote katika vikao vya mapendekezo ya bei, huduma ya maji safi na salama inahitajika zaidi na kuna gharama zake ikiwemo umeme na dawa za kutibu Maji” alisema Aweso


Share.

Leave A Reply