Monday, June 24

Vijana watakiwa kutumia kilimo kujiajili

0


Kikundi cha vijana ‘tubadilike’ kinachojishughulisha na kilimo cha mihogo katika kata ya kyamulaile kijiji mashule katika harmashauri ya Bukoba kimewataka vijana wa maeneo mengine kutumia nguvu zao kutengeneza ajira na kujipatia kipato na kuachana na dhana ya kukaa vijiweni wakisubiri ajira za kuajiriwa na mtu, kampuni au serikali.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti Wa kikundi hicho bw, Elipidius Benezethi wakati kikundi hicho kilipotembelewa na mwenyekiti Wa halmashauri hiyo Mh, Murushidi Ngeze ili kujionea vijana wa kikundi hicho wanatumiaje mkopo wa milioni nane waliopewa na halmashauri hiyo bila riba ukiwa na lengo la kuboresha kilimo chao cha muhogo na kuwawezesha vijana hao kupata nyenzo za kutumia katika kilimo hicho.

Kikundi hicho chenye jumla ya vijana 9 kina hekali 9.5 za kilimo cha muhogo ambapo wanatumia jembe la mkono ili kufanikisha kilimo hicho na kuhakikisha wanakuza shamba hilo. Mbali na changamoto hiyo kikundi hicho kimemuomba Mh, Ngeze kupatiwa komputa mpakato kwa ajiri ya kutunzia kumbukumbu zao na kwamba wao malengo yao siyo kuuza muhogo tu na mbegu bali ni kuchakata kabisa muhogo na kutengeneza kiwanda moja kwa moja.

Mh, Ngeze pia amekagua ujenzi wa vyumba viwili vya shule ya masingi Omukihisi ambapo amekuta ujenzi huo unaendelea vizuri.


Share.

Leave A Reply