Thursday, February 21

Red cross yatoa onyo kwa Watu wanaotumia vibaya nembo yao

0
Na Thabit Madai

Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Red Cross)  Mwadini Abass Juma amesema kumekuwa na baadhi ya watu wanatumia nembo ya Red Cross kinyume na utaratibu jambo ambalo ni kosa kisheria.

Hayo ameyaeleza wakati wa akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa elimu ya matumizi bora ya nembo ya Red Cross yaliyofanyika Shangani mkoa wa  Mjini  magharib Unguja.

Mwadini Amesema nembo hiyo imekuwa ikitumiwa visivyo halali na watu ambao sio wahusika wa Red Cross na kuitumia sehemu isiyo sahihi ikiwemo kujaribu kupoteza uhalisia wake.

 Ameeleza kuwa kutokana na matumizi holela ya Nembo hiyo Red Crossimekuwa ikitoa elimu kwa jamii katika mazingira mbalimbali ili kuona kuwa nembo hizo hazitumiki kiholela.

Aidha Rais huyo ameeleza kuwa Red Cross itaendelea kuhakikisha inatoa elimu kwa jamii ili kutoingia makosani.


Share.

Leave A Reply