Wednesday, August 21

RC awapiga marufuku wafanyabiashara wasio na vitambulisho

0


Na Mpitanjia, Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge amewapiga marufuku wafanyabiashara wote wasio kuwa na vitambulisho kuendelea kufanya biashara katika maeneo yote Mkoani humo.

Aidha wafanyabiashara waliokwisha nunua vitambulisho wametakiwa kuhakikisha wanakuwa navyo katika sehemu zao za kazi muda wote huku wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wakipaswa kusimamia suala hilo sambamba na kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao.

Dkt Mahenge ameyasema hayo hii leo wakati wa ziara aliyoifanya katika soko la Bonanza na Chang,ombe jijini Dodoma iliyokuwa na lengo la kugagua na kujionea hali ya wafanyabiashara walio na wasio na vitambulisho.

Pia kuhusu suala la usafi wa Soko Mkurugenzi wa jiji Godwin Kunambi amesema kila sehemu wakubaliane na viongozi wao namna ya kufanya lakini kwa hivi sasa mfanyabiashara atakaye kata kitambulisho hatotakiwa kulipia gharama ya shilingi mia mbili iliyokuwa ikichukuliwa kama tozo ya Halmashauri.

Nao wafanyabiashara Hassan Farahan na Joyce Mushi wakizungumza na chombo hiki wamempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wa kuwatambua kupitia vitambulisho hivyo na kuahidi kuyatekeleza maelekezo ya Mkuu wa Mkoa.

Katika ziara hiyo wafanyabiashara wengi wameonekana kutokuwa na vitambulisho ambapo hata hivyo baada ya kupewa elimu wameahidi kununua kwa manufaa yao binafsi.


Share.

Leave A Reply