Saturday, August 17

Mwanamitindo wa kiume afariki wakati akifanya onyesho la mavazi

0


Mwanamitindo wa kiume wa miaka 26 amefariki alipokua akifanya onyesho la mavazi katika tamasha la mitindo la São Paulo.

Tales Soares aliripotiwa kuanguka baada ya kutegwa na kamba za viatu alivyokuwa amevalia.

Waliyohudhuria tamasha hilo awali walifikiria kuanguka kwake kulikua sehemu onyesho lake.

Lakini walishtukia amebebwa kutoka ukumbini hapo na walinda usalama akiwa ameziraia.

Alipelekwa hospitali lakini madktari hawakuweza kuyaokoa maisha yake.

Kanda za video zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinamuonesha Soares akitembea kwa mwendo wa madaha kisha akageuka na kuangalia nyuma kabla ya kupatwa na kisunzi na kuanguka chiini

Waandalizi wa tamasha hilo wamethibitisha kifo chake katika mtandao wa Twitter lakini hawakutoa maelezo yoyote.

“Tunasikitika kumpoteza Tales na tunatuma rambi rambi zetu kwa familia yake,” ilisema taarifa yao”.

Saa kadhaa kabla ya mkasa huo modo huyo, aliweka picha zake kwenye akaunti yake ya Instagram ana kuzunzummzia tamasha hilo.


Share.

Leave A Reply