Sunday, August 18

Msuva aweka rekodi mpya ya mabao Morocco

0


Mshambuliaji wa Difaa El Jadida ya Morocco, Simon Msuva ameweka rekodi mpya ya mabao katika klabu yake baada ya kufunga mabao 12 msimu huu.

Msuva ameweka rekodi hiyo ya mabao na kuipita ile ya msimu uliopita baada ya juzi Jumamosi kufunga mabao mawili dhidi ya MAT Tetouan, Difaa walishinda mabao 2-0.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, amevunja rekodi yake ya mabao ya msimu uliopita ndani ya kikosi hicho ambapo alimaliza akiwa na mabao 11.

Kwa sasa Msuva anashika nafasi ya tatu katika listi ya wafungaji wa Ligi Kuu Morocco akiwa na mabao 12. Anayeongoza ni Mtogo, Kodjo Laba wa RSB Berkane aliyefunga mabao 17.


Share.

Leave A Reply