Sunday, August 25

Man City yaichapa Man United mabao 2-0

0


Timu ya Manchester City imewanyuka wapinzani wao wa jadi, Manchester United mabao 2-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Matokeo hayo yameiumiza timu ya Liverpool, ambayo ni mahasimu wa Manchester United kwani sasa wameshuka hadi nafasi ya pili ya msimamo wa ligi wakiwa na pointi 88 na kuzidiwa pointi moja na Manchester City.

Hatua hiyo sasa inaiweka katika nafasi nzuri ya ubingwa Manchester City kwani sasa ikishinda mechi tatu zilizobakia itajihakikishia ubingwa kwani itafi kisha pointi 98 ambazo haziwezi kufikiwa na Liverpool.


Share.

Leave A Reply