Thursday, August 22

Maambukizi ya Malaria yatajwa kupungua kwa asilimia 50

0


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,amesema kuwa Serikali imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.

Hayo ameyasema leo  wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya ya  Dodoma.

Aidha,amesema kuwa halmashauri kutenga fedha za ndani kwa ajili ya kununua viuwadudu ikiwa ni katika kupambana na maambukizi ya Malaria katika maeneo yao.

Waziri Ummy amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 2 ya utawala wa Rais John Magufuli, Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya Malaria kwa asilimia 50 kutoka wastani wa asilimia 14 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 7.

Hata hivyo amesema kuwa serikali imekuwa na mikakati mingi ya kupambana na maambukizi wa ugonjwawa malaria ambayo yamekuwa ikiuwa Watanzania wengi kuwa mbali na kugawa vyandarua pia wanapulizia dawa katika mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi.

”Serikali imenunua takribani lita 60,000 ya viuawadudu kwa ajili ya kuua mazalia ya mbu na kuzigawa katika mikoa yenye maambukizi makubwa ya malaria kama vile Mkoa wa Kagera, Geita, Kigoma, Lindi na Mtwara lakini pia niwaombe wananchi kutunza mazingira ili kujiepusha na mbu waenezao malaria,” amesisitiza Mwalimu

 Aidha, Mwalimu alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 angalau wajawazito 80 kati ya 100 waweze kuhudhuria kiliniki angalau mara nne hivyo kutoa fursa ya kufanyiwa vipimo mbalimbali ikiwamo malaria.


Share.

Leave A Reply