Monday, August 19

Lady Jaydee na Mwana FA kupanda jukwaa moja

0


Baada ya kuurudisha ushikaji wao uliopotea kwa muda mrefu, Lady Jaydee na Mwana FA watapanda katika jukwaa moja kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Wawili hao watatumbuiza katika tamasha la Anaweza lililoandaliwa na Jaydee ambalo itafanyika Machi 31 mwaka huu katika ukumbi wa Golden Tulip, Oysterbay.

Jide na Mwana FA walionekana kwa mara ya kwanza kwenye picha ya pamoja waliyopiga wakiwa studio Novemba 16 mwaka jana ikiwa imepita miaka mingi tangu walipoonekana wakiwa karibu.

Wasanii wengine ambao watatumbuiza kwenye tamasha hilo ni Domokaya, Bushoke, Alawi Junior na Nikki Mbishi.Read More

Share.

Comments are closed.