Wednesday, August 21

Kinamama msiwape watoto wachanga asali – Pinda

0


Waziri mkuu mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda amewatahadharisha wakinamama kuwa makini na matumizi ya asali kwa watoto wachanga,kwa kuwa utumbo wa mtoto unakuwa hauko tayari kuchakata vyakula kama asali.

Ametoa rai hiyo wakati wa maadhimisho ya kwanza siku ya nyuki duniani ambapo amesisitiza umuhimu wa ufugaji nyuki ikiwemo mazao yatokanayo na sekta hiyo hususani asali.

Amesema asali imekuwa ikiwapatia kipato baadhi ya wafugaji huku akibainisha kuwepo kwa zana za kisasa za ufugaji wa nyuki ili kuboresha ubora wa asali.


Share.

Leave A Reply