Sunday, August 25

Idadi ya waliofariki, majeruhi wa ajali ya lori lililowaka moto Morogoro hii hapa

0


Majeruhi 6 kati ya 38 wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefariki dunia na kufanya idadi ya waliofariki hadi sasa kufikia 82

Majeruhi hao ni wa ajali ya moto iliyotokea Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka Moto.

Kati ya majeruhi hao 17 wapo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine 15 wakiendelea kupatiwa matibabu katika wodi ya Sewahaji.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha leo amesema kwa sasa wamebaki majeruhi 32.

Aminiel  ameomba watu kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwa kuwa bado kuna uhitaji mkubwa.


Share.

Leave A Reply