Friday, March 22

Faida za kutumia majani ya mpera katika mwili wa mwanadamu

0


Pamoja na wengi wetu kuendelea kupenda kula mapera, Je ulishawahi kujua pia kuwa hata majani yake pia ni dawa hasa pale ukiamua kuyatumia? Kama ulikuwa hujui basi nipo hapa ili niweze kukujuza kwa kina juu ya faida zitokanazo na matumiazi ya majani ya mpera kama ifutavyo:

1. Ukitengneza chai ya majani ya mpera vizuri inaponyesha kwa silimia zote  kifua na kikohozi, hivyo kama unasumbuliwa na kifua na kikohozi basi tumia chai ya majani ya mpera ili ujitibu.

2. Je tumbo lako linauma, kama jibu ni ndiyo basi majani ya mpera ndiyo tiba sahihi kwa ajili ya matatizo hayo, unachotakiwa kufanya ni kuchuma majani kadhaa ya mpera kisha kuyatafuna yenyewe.

3. Vilevile majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio (allergy).

4. Pia majani haya ya mpera yakichemshwa kama chai yanaondoa cholesterol iliyozid mwilini.

5. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango cha tatizo la sukari mwilini.

6. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.

7. Pia inatumika kama scrub ya uso. Chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi na inasaidia kuondoa uchafu usoni..

 8. Majani ya mpera yanajaza nywele na kurefusha nywele kwa watu wenye tatizo la kukatika kwa nywele, unasaga na kuchemsha kisha acha yapoe ndio upake kichwani kutoka chini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha ya nywele zako.


Share.

Leave A Reply