Tuesday, August 20

Diego Costa agoma kufanya mazoezi Atletico Madrid

0


Wiki iliyopita April 11 mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa alifungiwa kucheza mechi nane za La Liga kufuatia kumtusi mwamuzi Jesus Gil katika mechi yao dhidi ya Barca ambayo walipoteza kwa goli 2-0.

Mtandao wa AS umeripoti kuwa mchezaji huyo juzi Alhamisi aligoma kufanya mazoezi kufuatia klabu kutaka kumpa adhabu ya kinidhamu kwa kosa hilo lililompelekea kufungiwa mechi nane.

Pia imeelezwa kuwa mahusiano yake na klabu yameshuka ghafla na huenda ikapelekea kuondoka kwa Mhispania huyo majira ya kiangazi


Share.

Leave A Reply