Saturday, August 24

Breaking News: Zitto Kabwe aachiwa kwa dhamana

0


Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru kwa dhamana ya Polisi yenye thamani ya Milioni 50 muda huu baada ya kulala mahabusu tokea jana (Alhamisi) usiku.

Hayo yamebainishwa na Wakili wa Mbunge huyo ni Emmanuel Lazarus Mvula ambae ndie aliyemdhamini Zitto na kusema anatakiwa kuripoti katika kituo kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro siku ya Jumatatu Machi 12, 2018.

Mbunge Zitto Kabwe alikamatwa na Jeshi la Polisi la Mkoa wa Morogoro wakati akiwa katika muendelezo wa ziara yake iliyoanza Februari 19 akiwa pamoja na viongozi wengine wa ACT- Wazalendo wa malengo ya kushiriki kazi za maendeleo na kuzungumza na kamati za maendeleo za kata hizo.Read More

Share.

Comments are closed.