Thursday, July 18

BREAKING NEWS: Zitto afikishwa Mahakama ya Kisutu

0Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu .

Taarifa iliyotelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ado Shaibu bila kueleza sababu za kufikishwa kwake Mahakamani hapo, akitokea kituo cha Polisi Mburahati.

“Zitto anapelekwa Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kisutu muda huu akitokea kituo cha Polisi Mburahati,” amesema Ado katika taarifa hiyo.

Ikumbukwe Zitto anashikiliwa kwa kile alichodai idadi ya watu 100 waliouawa Kigoma katika Mkutano wake na waandishi wa habari ulifanyika wiki iliyopita.

Share.

Leave A Reply