Monday, June 17

Vijana 133,820 wapelekwa Jeshini kwa lazima nchini Morocco

0


Vijana wote nchini Morocco sasa watapitia mafunzo ya kijeshi ya lazima baada ya mpango huo uliotangazwa na serikali ya nchi hiyo mwaka wa 2006 kuanza mwaka huu.

Jumla ya vijana 133,820 raia wa Morocco wamesajili kwa mpango huo, ikiwemo wasichana 13,614- hii ni kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani.

Wizara hiyo imeongeza kwamba vijana hao walijisajili kwa hiari yao. Kwa mujibu wa bajeti ya nchi hiyo ya 2019, vijana 40,000 wa kike na kiume wenye umri kati ya miaka 19-25 watashiriki mazoezi hayo mwaka huu kwa muda wa miezi 12.


Share.

Leave A Reply