Saturday, August 17

VIDEO: Wafanya kazi zaidi ya miaka 15 bila mishahara

0


Waliokuwa wafanyakazi (Madereva) wa Kampuni ya ‘WHITE STAR’ ambayo wanajihusisha na usafirishaji wa mafuta nje ya Nchi, wamemlalamikia aliyekuwa mwajiri wao kwa kuwachafua mitandaoni kwa kuwachapisha katika matangazo na kusema kuwa ni wezi na wanatafutwa na polisi kitendo walichokiita ni udhalilishwaji, wamesema kwa wameitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 15 pasipo kulipwa mishahara na kupewa mikataba, pia wamesema katika jarida alilowafungulia katika kituo cha polisi mwajiri huyo anasema madereva hao walimuibia mafutalita 2000 kwa kila dereva toka walipoanza kazi hadi sasa, hivyo madereva hao wamemuomba mwajiri huyo kuwaomba radhi kwa kuwadhalilisha.

Mtandao huu umefanya jitihada za kuwatafuta wahusika katika Kampuni hiyo ilikusikiliza upande wao lakini jitihada hizo ziligonga mwambabaada ya mulizi kutuambia kuwa hakuna mtu wa kulizungumzia jambo hilo.

ANGALIA FULL VIDEO HAPA CHINI…..USISAHAU KUSUBSCRIBE…..


Share.

Leave A Reply