Wednesday, August 21

Lwandamina kuwasili singida kesho Kupambana na singida United kwaajili ya kombe la FA

0


Kocha Mkuu wa kikosi cha Yanga, George Lwandamina, anatarajiwa kuwasili mjini Singida kesho kwa ajili ya mechi ya Kombe la FA dhidi ya Singida United.

Lwandamina alisalia jijini Dar es Salaam wakati kikosi kikianza safari ya kuelekea Morogoro kuweka kambi ya muda mfupi kuelekea mchezo huo.

Wakati huohuo kipa namba mbili wa Yanga, Ramadhan Kabwili, naye ataondoka sambamba na Kocha wake Lwandamina kuelekea mkoani Singida.

Kabwili alishindwa kujumuika na wenzake kwenye safari ya pamoja kuelekea Morogoro kutokana na majukumu ya kukitumia kikosi cha timu ya Taifa, Ngorongoro Heroes iliyocheza dhidi ya Congo leo.
Read More

Share.

Comments are closed.