Wednesday, May 22

BREAKING: Gari lagongana na treni Tanga, mmoja afariki

0


Mtu mmoja amefariki na wanafunzi 19 kati ya thelathini wamejeruhiwa baada ya gari la abiria lenye namba za usajili T930 DML aina ya Costa  walilokuwa wakisafiria kupata ajali.

Watu hao walikuwa wakienda kucheza mpira na gari walilokuwa wakisafiria kuligonga Treni eneo la Gofu jijini Tanga.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga SACP Edward Bukombe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Endelea kufuatilia Muungwana Blog kwa habari zaidi kuhusu ajali hiyo.


Share.

Leave A Reply