Wednesday, August 21

Zifahamu sura mbili ziletazo mafanikio

0Kila kitu unachokiona katika dunia hii kipo katika mwenekano wake. Na mwenekano huo ndio ambao hufanya viumbe vyenye akili viweze kutambuana kwa kutumia muonekanao huo. Pia mwonekano huo ndiyo hutumika kijenga picha kamili ya kitu halisi.

Kama ndivyo hivyo basi katika kuyasaka mafanikio inahitajika mtu husika aweze kuvaa sura mbili ili kuyanasa mafanikio hayo. Na sura hizo mbili ndizo zitakazokufanya wewe uweze kujitofautisha na watu wengine.

Huenda ukawa hujanielewa bado usipate shida  ipo hivi sizingumzii umbo wala muonekano ulionao ndio utaokupa mafanikio laa hasha. Bali nazungumzia ya kwamba ili uweze kupata mafaniko yako unatakiwa kuwa na sura ya Mwalimu na sura Mwanafunzi pia.

Ninapozungumzia suala la kuvaa sura ya mwalimu, kwanza tambua ya kwamba mwalimu si yule anayefundisha darasani pekee yake la hasha, bali mwalimu mzuri ni yule aliyelewa kisha kuyafanyia kazi yale ambayo amelewa kisha kuwafundisha wengine.

Hii ina maana ya kwamba kile kidogo ambacho unakifahamu kisiwe siri yako bali weka mikakati thabiti ambayo watu wengine wataweza kunufaika na hicho unakijua. Huenda kwako ukakiona ni kidogo sana ila tambua ya kwamba wapo baadhi ya watu kwa hicho unachokijua japo wewe unakiona ni kidogo kwao ni kitu kikubwa sana.  Hivyo kila wakati jifunze kuwa mwalimu kwa watu wengine.

Sura ya pili ambayo unatakiwa kuwa nayo ni sura ya mwanafunzi. Pamoja na kuwa mwalimu lakini elimu haina mwisho hivyo endelea kuwa mwanafunzi , huku ukizingatia ya kwamba mwanafunzi bora ni yule ambaye yupo tayari kujifunza katika mazingira yeyote yale.

Lakini mwanafunzi huyu ili awe mwanafunzi ni lazima pawepo na utayari kutoke ndani ya nafsi ya mtu husika, kwani kama mtu atalazimishwa kujifunza atashindwa kuyafanyia kazi yale ambayo amejifunza.

Lakini pia mwanafunzi makini ni yule mwenye kutambua ni nini maaana ya uanafunzi, yaani awe tayari kulipa gharama ya pesa na gharama ya muda kwa kitu anachotaka kukifahamu. Kufanya hii ndiyo nguzo ambayo kila unayemuona ana mafanikio imemsadia kwa namna moja ama nyingine kuwa hivyo alivyo leo.

Kila kitu ambacho unakiona mbele ya macho yako tambua kuwa kuna mtu aliwekeza gharama fulani katika kitu hivho, hadi kupelekea kitu hicho kuwa hivyo kilivyo leo.

Hivyo ndugu yangu naomba nikwambie ya kwamba mafaniko ya kweli yanajengwa na sura hizo mbili ambazo nimekwisha kukueleza yaani kuwa mwalimu lakini pia kuwa mwanafunzi. Ukiyazingatia hayo utaishi maisha yenye tija katika sayari hii ya dunia.


Share.

Leave A Reply