Sunday, April 21

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo afanya mazungumzo na mwanamfalme wa Saudi Arabia

0


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amekutana na kufanya mazungumzo na mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman ambapo wamekubaliana juu ya umuhimu wa kutekeleza makubaliano ya Sweden yanayohusu kusitishwa kwa mapigano na kurejeshwa kwa amani nchini Yemen.

Waziri huyo wa Marekani yuko nchini Saudi Arabia ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika eneo la Ghuba huku kifo cha mwanahabari Jamal Kashoggi na kutengwa kwa nchi ya Qatar zikitajwa kuwa ajenda kuu za ziara yake.

Akiwa nchini Qatar, Mike Pompeo amezitaka nchi jirani na taifa hilo kusitisha hatua yao ya kuitenga Qatar ili kupatikana kwa muafaka wa mgogoro uliodumu kwa takriban miezi 19. Mataifa ya Saudi Arabia, Bahrain, Misri pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu walikubaliana kuitenga Qatar kwa tuhuma za kufadhili makundi ya kigaidi na kuingilia mambo ya ndani ya mataifa hayo.

Hata hivyo Waziri huyo wa Marekani amelazimika kusitisha ziara yake na anatarajiwa kurejea nyumbani kwa lengo la kushiriki msiba wa kifamilia.


Share.

Leave A Reply