Friday, July 19

Waitara awapa onyo watakaotaka kumkwamisha katika Uwaziri wake

0


Naibu waziri mteule wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mwita Waitara amesema atashirikiana na kila mtu katika utekelezaji wa majukumu yake na wale watakaobainika kumkwamisha atakabiliana nao.

Waitara ambaye Leo Jumatatu Novemba 12, 2018 atakuwa miongoni naibu mawaziri na mawaziri watakaoapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuteuliwa  Jumamosi amesema ingawa bado majukumu yake hajakabidhiwa kwa sababu hajaapishwa lakini hatokubali watu wamkwamishe katika utendaji kazi wake.

Mteule huyo amesema hayo Jumapili alipozungumza na Mwananchi akisema, “Awe mpinzani au mtu yeyote sitokubali anikwamishe. Ninaahidi kushirikiana na kila mtu na namshukuru Mungu kwa nafasi hii na nitaitumikia kwa moyo wangu wote.

Ki msingi sikutarajia kama nitateuliwa kwa sababu sikujua kama Rais John Magufuli atafanya mabadiliko madogo katika mabaraza lake la mawaziri,” amesema Waitara ambaye ni Mbunge wa Ukonga aliyejizulu ubunge akiwa Chadema na kuhamia CCM alipoteuliwa kugombea na kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi uliofanyikia Septemba 17, 2018


Share.

Leave A Reply