Sunday, August 18

VIDEO: Ajali mbaya ya gari yaua, RPC na mashuhuda wasimulia A-Z

0


Watu 2 wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili madogo katika eneo la Oldonyosambu wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Akithibitisha ajali hiyo kamanda wa polisi Mkoani Arusha Jonathani Shanna amesema kuwa ajali hiyo imetokea katika barabara ya Arusha Namanga majira ya saa 9 alasiri ya leo.

Amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari iliyokuwa nyuma ilikuwa inataka kuipita gari iliyokuwa mbele yake hivyo kupelekea kugongana na kusababisha ajali hiyo.

Akitaja majina ya Marehemu amesema kuwa mmoja kati yao ni raia wa Kenya ajulikanae kwa jina la Onesmo Mwangi na Mtanzania ajulikanae kwa jina moja la Henry.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI……USISAHAU KUSUBSCRIBE


Share.

Leave A Reply