Wednesday, July 17

Trump na Netanyahu wafanya mazungumzo kuhusu Iran

0


Rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wafanya mazungumzo kuhusu Iran.

Msemaji wa ikulu ya Marekani, Judd Deere ametoa taarifa ya maandishi kuhusiana na mazungumzo ya Trump na Netanyahu.

Katika taarifa hiyo Deere amesema Rais Trump na waziri mkuu Netanyahu wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na wamekubaliana kushirikiana kuizuia Iran isilete madhara yeyote pamoja na kutetea maslahi yao ya pamoja.


Share.

Leave A Reply