Saturday, August 17

Rais Erdoğan akemea vikali mashambulizi yaliolenga makanisa nchini Sri Lanka

0


Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan akemea vikali mashambulizi  ya kigaidi yaliolenga makanisa nchini Sri Lanka

Watu zaidi ya 156  wameuawa na wengine  zaidi ya 500 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya kigaidi yaliolenga makanisa na nyumba za wageni nchini Sri Lanka.

Mashambulizi hayo yametekelezwa wakati ambapo wakristo walisherehekea siku kuu ya Krismas.

Katika ukurasa wake wa Twitter, rais Erdoğan  amekemea mashmbulizi hayo na kusema kuwa yamelenga ulimwengu mzima.

Mashambulizi hayo yamelenga  majumba matatu ya kfaghari ya kopokea wageni na makanisa matatu mjini Colombo.

Nchini Sri Lanka  wakristu ni asilimia 7, wabudha asilimi 70, wahindu  asilimia 12 na waislamu asilimia 10.


Share.

Leave A Reply