Thursday, February 21

Kuna Tofauti Gani kati ya Kupenda na Kutamani?

0


Hapo zamani kulikwepo na Mwalimu mmoja anayejulikana mpaka leo hii, aitwaye Buddha. Kutokana na busara zake na hekima zake, alifahamika na wengi na alikuwa akitembelewa na watu mbalimbali wakiwa na maswali mbalimbali, kwa lengo la kumuuliza na kufahamu mengi.

Aliwahi kuulizwa, JE KUNA TOFAUTI GANI KATI YA KUPENDA NA KUTAMANI?

Buddha alijibu; “Ukiliona Ua zuri ukalitamani, utalichuma. Lakini ukilipenda utalimwagia maji, kuliwekea rutuba na kulijali ili lizidi kuchanua vyema”.

Jibu hilo ni fumbo tosha kabisa kuonyesha utofauti uliopo kati ya kupenda na kutamani.

Vijana wengi wa sasa wanashindwa kutofautisha tofauti kati ya Kupenda na Kutamani na ndio maana Mahusiano ya Wakati wa sasa, mengi sio ya kudumu kwa wakati mrefu. 


Share.

Leave A Reply