Tuesday, August 20

Kanuni muhimu za mafanikio

0


“People may forget what you said, they also might remember not what you did, but never forget how you made them feel” msemo huo ukiwa na maana ya kwamba watu wanaweza wakasahau ulichosema, wakasahau kabisa ulichowafanyia lakini kamwe hawezi kusahau ulivyowafikirisha kihisia” mwisho wa kunukuu.

Lugha yetu tamu ya kiswahili ina misemo mingi mno yenye kujenga na kuimarisha fikra zetu. Basi kwa ajili hiyo hiyo nakusihi ambacho utakwenda kusoma katika makala haya uweze kukiweka katika hisia zako maana hisia zina nguvu sana, hisia ndizo ambazo huisukuma akili katika kutenda.

1. Chukia hali uliyonayo.
Tafiti zinatuambia ya kwamba moja ya sifa ya mwanadamu ni kwamba ana tabia ya kuridhika sana na hali ambayo aliyonayo. Tafiti hizohizo zinaendelea kueleza ya kwamba watu wengi wakipiga hatua ya jambo lolote lile huwa wanaridhika nalo kwa asilimia mia moja.

Kuridhika huko huko kunafanya watu wengi ambao kwa namna moja ama nyingine ambao waliweza kufanikiwa kwa kiwango fulani kupoteza ubora wa kiutendaji, hii ina maana ya kwamba kuridhika na hali iliyonayo kwa namna yeyote ile uliyonayo ni adui wa Mafanikio yako.

Hata hivyo ni kwamba hauna haja hata chembe ya kuikubali hali iliyonayo. Hii ni kiwa nina maana ya kwamba hata siku moja usiridhike mahali ulipo leo, ni vyema uendelee kuona kiu yako mafanikio bado haijakamilika hata kama ni kweli umeanza kufanikiwa. Kwa mfano wewe ni mfanyabiashara hata uwe unauza kiasi gani cha fedha, hebu ona kiasi hicho bado hakitoshi.

Vilevile katika kuchukia hali uliyoayo ni lazima uwe wa kwanza kuzungumza kuhusu wewe, kuzungumza kuhusu wewe ni lazima kinywa chako kiseme vitu chanya tu, mfano wa maneno hayo ni kama vile Mimi ni tajiri, Mimi naweza, mimi ni mshindi wa maisha yangu kwa kile ambacho nakifanya na maneno mengine yaliyo chanya kama hayo,  kama mara kadhaa nilivyozoea kukukumbusha ya kwamba kusema pekee haitoshi Bali unahitaji hatua madhubuti za kiutendaji.

2. Jipe cheo.
Unashangaa wala huna haja ya kushangaa, upo sahihi kwa hicho ambacho unakisoma, ni kweli jipe cheo kwa kazi ambayo unaifanya. Hapa nazungumza na wewe ambaye hutaki cheo cha kupewa na mtu. Hebu tujiulize wale ambao ni baadhi ya maskofu, manabii, wakurugenzi na waanzilishi wa makampuni wao vyeo hivyo walipewa na nani kama sio wao wenyewe.

Ipo haja ya wewe leo kujipa cheo ya kazi ambayo unaifanya. Kama wewe una uwezo wa kufaulu somo la hesabu unaweza ukajiita Mathematics Master (M.M), Kama wewe ni mkulima wa kilimo cha matikikiti unaweza ukajiita (Mtalamu Wa matikikiti Tanzania nzima) na vyeo vingine vingi kulingana na kazi ambayo unaifanya. Pia lazima kama umefungua mahali fulani ambayo unafanyia kazi ni lazima pawe na  jina ambalo litawavutia wateja.

Cheo pekee yake hakitoshi tafuta jina jingine nzuri la kuipa ofisi yako kama unayo. Suala hili la kuipa ofisi jina lako huwa namkumbuka sana rafiki ya issa alimaarufu kissmchapakazi kuna siku alinipeleka kwa mama mmoja ambaye anauza mkaa, ila kitu ambacho kilinifurahisha kutoka kwa mama yule nilikuta banda lake ambalo analiuzia mkaa amelipa jina la “Mkaa Plaza” maneno hayo yanaonekana kwa nje ya banda hilo, kiukweli jina hilo lilinifurahisha sana, sio jina tu ambalo linifanya nitoe tabasamu langu bali huduma ambayo inatolewa na mamab yule.

Isionekane nampigia sana debe mama huyo, la hasha ila maana yangu ni kwamba tafuta jina linakalo kutambulisha kwa wateja wako, sio jina tu ambalo litakutambulisha sokoni bali utoaji wa huduma bora tofauti na wengine ndio ambao utakufautisha na wengine. Endapo utayanya hayo hauna haja ya kupeleka hirizi tena biahara yako bali wateja watakuja wenyewe. Si kwenye biashara tu ndiko kunakohitaji ubunifu  Bali kwa kila jambo ambalo unalifanya ni lazima ubunifu utumike, ubunifu huo ndio ambao utaokutafutasha na watu wengine katika jamii.

Bila shaka umenielewa vyema kwa hayo machache kati ya mengi ambayo yana maana pana sana katika kugeuza sayari ya kulalamika na kukupeleka katika sayari ambayo ni ya mafaniko yako

Na: Benson Chonya.


Share.

Leave A Reply