Monday, August 19

Jinsi ya kuwa mzungumzaji bora

0


Wapo baadhi ya wasomaji wangu walikuwa wakiniuliza “eti nifanye nini ili kuwa mzungumzaji mzuri mbele ya watu wengine?  Swali hili kiukweli limekuwa likiwatatiza watu wengi sana kwa namna moja ama nyingine.  Na kutokana na hali hiyo kumewafanya watu hao hao kuwa katika hali unyonge,  kwani huisi watachekwa na sababu nyingine kama hizo.

Lakini ukweli ni kwamba endapo utazijua siri hizi kuwa mzungumzaji bora zitakwenda kukusaidia kutoka katika hali uliyonayo hatimaye kuwa mzungumzaji mzuri.

Zifuatazo ndizo mbinu kuwa mzungumaj bora:

1.kuwa na taarifa za uhakika na kutosha.
Moja ya  njia bora ya kuwa mzungumzaji mzuri ni kuwa na utajiri wa vitu vingi katika kibubu cha ubongo wako . Watu wengi wanajiona hawawezi kuchangia maada yeyote ile mbele ya wengine hii ni kwa sababu wamekuwa hawana taarifa sahihi na za uhakika za kuweza kuzungumza. Hivyo Kama endapo nia yako ni kutaka kuzungumza mambo mbalimbali katika jamii yako ni lazima ujue vitu hivyo kwa undani zaidi.

Kama unataka kuwa mzungumzaji juu ya masuala ya michezo ni lazima uweze kufutilia taarifa mbalimbali za michezo kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo hutoa taarifa za michezo. Kutokuwa na taarifa nyingi za kutosha zimefanya watu mbalimbali kufanya vitu vile vile kila wakati.

Watazame wasanii mbalimbali katika nchi wameshindwa kuwa wabunifu katika kazi zao kwa sababu waliyonayo wanahisi yanatosha.  Ila ukweli ni kwamba kujifunza vitu vipya hakuna mwisho. Na daima kumbuka ule usemi usemao “no research no right to speak” kama hauna utafiti wa kutosha huna haki ya kuzungumza, hivyo ukitaka kuwa mzungumzaji mzuri ni lazima ufanye utafiti wa kutosha juu ya jambo hilo.

2. Lazima uwe msikilizaji mzuri.
Hii pia ni siri mojawapo ya kuwa mzungumzaji mzuri mbele ya watu wengine. Huwezi kutaka kuwa mzungumzaji bora kama hujui kusikiliza. Matokeo ya kuzungumza chanzo chake hutokana na kusikiliza vizuri anachokizungumza mtu mwingine.

Pia tatizo hili la kutojua kusikiliza limekuwa likiwaathiri watu wengi sana.  Kwa tafiti zinaonyesha ya kwamba msikilizaji ndiye ambaye hutumia nguvu nyingi katika kuelewa kuliko mzungumzaji.  Kama ndivyo hivyo hakikisha unatumia nguvu nyingi sana katika kusimamia akili yako katika kusikiliza, kama kweli unahitajj kuwa mzungumzaji mzuri.

3. Kujiamini
Suala kubwa ambalo limekuwa likiwaathiri watu wengi katika kuzungumza ni kushindwa kujiamini. Wengi wamejenga na hofu ambayo imekuwa haiwasaidii.  Wengi huona ya kwamba Watachekwa, watazomewa na vitu vingine vingi kama hivyo. Lakini hali hii imekuwa ikizuka kwa baadhi ya watu ambao kwa asilimia kubwa imejengeka tangu wakiwa wadogo.

Na hofu hiyo umekufanya ujione mnyonge sana,  hata wakati mwingine umekuwa ikihisi huna thamani mbele ya watu wengine. Ila nichotaka kukwambia njia bora ya kuondokana na hofu hiyo uliyonayo ni kufanya kitu ambacho unakiogopa.  Kama umekuwa unashindwa kuzungumza mbele za watu anza leo. Kwani kama nilivyosema hapo awali njia bora ya Kuwa mtu mwenye mafanikio ni kufanya kitu ambacho unakiogopa.

4. Anza kufanya mazoezi ya kuzungumza.
Jambo la nne na la mwisho ambalo nilipanga kuzungumza nawe siku ya leo ni kuanza kufanya mazoezi ya kuzungumza .  Huwezi kuwa mzungumzaji bora kama hutaki kufanya mazoezi ya kuwa hivyo inavyokata. Hivyo mazoezi ni chanzo cha ushindi. Kama ilivyo kwa wachezaji wa mpira kama hawajaanza kucheza mechi ni lazima wafanye mazoezi. Hivyo hata wewe unahitaji kutenga  walau nusu saa ya kuzungumza.  Unaweza ukachugua maada fulani na ukafanya mazoezi angalau nusu saa ya kuzungumza maada hiyo ukiwa peke yako.

Endapo utafanya hivyo kutakusaidia kujenga uwezo wa kukufanya uwe mzungumzaji mzuri kwa watu wengine.

Yawezekana kabisa suala hili la kutokuwa mzungumzaji linakuhusu wewe ambaye unasoma makala haya,  nichotaka kukwambia kila kitu kinawezekana na utakwenda kuwa mzungumzaji mzuri mbele ya watu wengine endapo tu yote ambayo nimeyaeleza utaamua kuyafanyia kazi.Read More

Share.

Comments are closed.