Tuesday, August 20

Jambo la kulitafakri kwa undani kabla ya kuingia katika maisha ya ndoa

0


Kabla ya kuingia kwenye maisha ya ndoa unatakiwa kupanga namna ambavyo utaishi kwenye ndoa hiyo hii ni kwa sababu waafrika ni kawaida yetu kuishi pamoja na ndugu zetu na kusaidiana katika mambo mbalimbali ya maisha tunapokuwa ndoani. Sio jambo geni kumkuta kijana au msichana anaishi na wadogo zake na kuwasomesha.

Linapokuja suala la ndoa ni vyema jambo hili likawekwa sawa mapema baina ya mume na mke kwa kujiuliza mambo yafutayo je mtaweza kuishi na ndugu wangapi? Na wa upande upi na kwa kigezo gani? Je wataanza kuishi nanyi muda gani baada ya kuoana?  Hili ni jambo muhimu la kuwekana wazi kabla humjaamua kufanya hivyo.

Lazima mtafakari jambo hili pale tu mtakapooana. Hili si jambo dogo na linaweza kuharibu amani kabisa ndani ya nyumba kama hamtakaa pamoja na kupanga juu ya jambo hili. Ni vyema mkaliweka sawa mapema na wale mnaoishi nao wajue hawaishi tena na kaka au dada bali Mr & Mrs hivyo heshima iwe kwa wote.

 Pia sishauri kuishi nao mara tu baada ya kuoana, ni bora wakaenda kwa ndugu wengine angalau mwezi mmoja wa kwanza muweze kuwa na wakati wenu wa faragha wa kufahamiana vizuri na kuizoea nyumba yenu mkiwa wenyewe.

Hili ni jambo muhimu sana la kupanga kabla ya kuingia mazima katika ndoa yenu, kwani msipanga mapema juu ya jambo hilo la kuishi ndugu ni lazima ndoa yenu haitakuwa na amani na mitafaruko ya hapa na pale itakuwa upande wenu.


Share.

Leave A Reply