Thursday, July 18

Giza nene latanda Argentina

0


Rais wa Argentina, Mauricio Macri amesema chanzo kilichosababisha kukatika kwa umeme katika sehemu kubwa ya nchi hiyo hapo jana bado hakijafahamika.Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo haswa cha tatizo.

Macri ameyasema hayo kupitia ukarasa wake wa mitandao ya jamii, aliandika kwamba tatizo la ufundi katika mfumo wa umeme lilipelekea tatizo la umeme nchi nzima, mpaka sasa tatizo haswa bado halijafahamika.

Jana kuanzia mida ya asubuhi karibu nchi nzima ya Argentina hakukuwa na umeme tatizo lililodumu kwa karibu masaa 7.


Share.

Leave A Reply