Thursday, August 22

Athari za mwanamke kushindwa kufika kileleni na chanzo chake

0TATIZO hili la mwanamke kutofikishwa kileleni wakati wa kujamiiana huitwa ‘Female Orgasmic Disorders’ kufika kileleni tunaita ‘orgasm’ au ‘climax’. Kila mwanamke ni lazima afike kileleni wakati wa tendo hili. Hii ni hali ya kimaumbile ambayo imeumbwa na Mungu.

Mwanamke hufika kileleni pale anapokuwa amesisimka kwa kiwango cha hali ya juu. Hali ya msisimko kwa mwanamke tunaita ‘sexual arousal’ na huanzaia pale mwanamke anapokuwa na hamu ya tendo hili la kujamiiana yaani ‘sixual desire’.Kwa kawaida msisimko hukolezwa wakati wa maandalizi ya tendo au ‘romance’ kwa kutumia milango mitano ya fahamu.

Kila mwanamke ana jinsi yake ya kusisimka wakati huu wa maandalizi kutegemea na aina ya mlango wa fahamu unaomsukuma, mfano kuona, kusikia, kugusa, kuonja na kunusa. Wapo wanawake wanaosisimka na mlango mmoja, wengine miwili au zaidi.

MAANA YA KUFIKA KILELENI

Tunaposema mwanamke au mwanaume amefika kileleni katika tendo ni pale amefika kiwango cha juu cha msisimko na raha katika tendo hilo. Mwanaume huanza kusisimka katika sehemu ya mbele ya dhakari na mwanamke huwa na sehemu maalumu.

Msisimko hubebwa na mishipa ya fahamu ya kiuno, uti wa mgongo hadi katika ubongo ambapo kiwango cha juu hufikiwa na mwanaume hutoa manii na mwanamke hutoa majimaji sehemu ya siri. Mwanamke hufikia mwisho wa tendo kwa muda huo lakini kutokana na hali ya kimaumbile mwanamke anaweza kuendelea na akafikia tena na tena kileleni.

Mwanamke ana sehemu maalumu ukeni ambazo zinapopata mguso na msuguano humwezesha afike kileleni. Sehemu hizi kitaalamu zinaitwa ‘Grafenberg Spot’ au G. spot. Sehemu hii inapatikana ukeni kwa ndani. Iligunduliwa miaka ya nyuma na daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama wa Ujerumani aitwaye Ernest Grafenberg.

Sehemu hii inamletea mwanamke msisimko wa nguvu na kumfanya amalizie raha yake ya kujamiiana kwa kishindo kikubwa ‘ Powerful Orgasm’ na kutoa majimaji ukeni ‘Female ejaculation’. Majimaji haya yanapomtoka mwanamke bado haijajulikana hasa yanatoka sehemu gani katika eneo hilo ingawa baadhi wanasema ni mkojo unatoka mara moja kwa kishindo, wengine wanasema yanatoka katika vitezi vidogo nyuma ya njia ya mkojo ‘Paraurethral ducts’ .

Vitezi hivi pia baadhi ya wataalamu huvifananisha na tezi dume kwa mwanaume, kwani kazi ya tezi dume ni kutoa majimaji au manii wakati wa kufikia mshindo au kilele. Ili kuamsha G. spot mwanamke afike kileleni inatakkiwa uume uwe na nguvu za kutosha vinginevyo ni vigumu kufikia hapo.

CHANZO CHA TATIZO

Chanzo kikuu kinachoweza kumsababishia mwanamke asifike kileleni au achelewe kufika hapo ni sababu za kimazingira na kisaikolojia, ‘Situational and Psychological factors’. Vile vile zipo sababu za magonjwa au mifumo ya mwili mfano, mfumo wa fahamu na homoni.

Kiasi kikubwa cha tatizo hili hutokana na matatizo yanayo-mzunguka mwanamke kama vile, maandalizi duni ya tendo la ndoa kwa kutozingatia kanuni na mwanamke kuingiliwa kabla ya kuwa tayari na hii inaweza kuwa ni kila mara.

Kutokuamsha viungo vyake vya uzazi kwa ajili ya tendo ‘Insufficient foreplay’, tatizo jingine ni wote wawili mume na mke kutojua mapenzi na kazi ya viungo vyao vya uzazi, kutofahamu aina au njia mbalimbali za romance hivyo kusababisha mgongano mengine ni kutoelewa au kupenda kama mwenzake anavyohitaji, matatizo au migongano katika mahusiano, kujihisi vibaya pale unaposhindwa kumudu tendo la ndoa, kuogopa kuachwa au kukimbiwa unapohisi hufurahii tendo na huwezi kufika kileleni, kulichukia tendo lenyewe hasa endapo ulishawahi kupata matatizo nalo kama kubakwa au kuingiliwa kinyume na maumbile, na endapo kama una matatizo mazito ya kisaikolojia mfano ‘Depression’.

ATHARI ZA TATIZO

Mwanamke ambaye hafiki kileleni wakati wa tendo la ndoa, yupo hatarini kupoteza hamu ya tendo la ndoa hivyo basi kukosa msisimko wa tendo na

ieleweke kwamba, mwanamke ambaye hafiki kileleni hupata hamu kama kawaida pale tatizo linapoanza , pia hupata msisimko ambao haufiki mshindo kutokana na kukatizwa na mumewe endapo mumewe anawahi kumaliza tendo, au na hali ya mazingira na kisaikolojia. Hali hii inapoendelea mara kwa mara mwishowe mwanamke huyu hupoteza kabisa uwezo wa kumaliza tendo kwa mshindo au kufikia kileleni yaani ‘climax’.

Tatizo linapoendelea husababisha mwanamke awe anapata maumivu wakati wa tendo la ndoa. Maumivu haya hutokana na woga au wasiwasi hivyo kusababisha uke uwe mkavu na misuli yake hubana hivyo hata uume unashindwa kupenya.

MATIBABU

Hufanyika baada ya uchunguzi wa kina katikaa hospitali ambapo vipimo mbalimbali vitafanyika. Daktari atakuelekeza njia mbalimbali za mguso wa kuamsha hisia na msisimko ili kukuwezesha kufikia kileleni na kurudisha furaha yako na kama hujawahi kuipata basi utaipata. Njia hizi ni njia ya kujiamsha mwenyewe hisia ‘ Self – stimulation,’ njia nyingine ni kama vile ‘Relaxation techniques’ na ‘Sensate focus exercises’.

Njia nyingine ni kupata elimu na upeo kuhusu mapenzi, tiba nyingine ni za kisaikolojia kutambua na jinsi ya kuepuka migongano katika mahusiano ya kimapenzi.


Share.

Leave A Reply