Sunday, August 18

TRA yajirudi kwa wafanyabiashara wa mikoa ya Kusini

0


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeagiza biashara zote, yakiwemo maduka yaliyofungwa na Mamlaka hiyo katika mikoa ya kusini Lindi na Mtwara zifunguliwe na kuendelea kuhudumia jamii ili serikali iweze kupata kodi yake.

Kamishina wa kodi ya mapato za ndani, Elijah Mwandumbya ametoa amri hiyo kwenye kikao cha pamoja kati yake na wafanyabiashara wa mkoa wa Lindi kilichofanyika mji humo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wao kwamba baadhi ya wafanyabiashara waliowengi, wakiwemo wa vifaa vya ujenzi, soda na vyakula katika mikoa hiyo, wamelazimika kuzifunga kwa madai kukadiliwa kodi kubwa tafauti na kile wanachokipata.

Akizungumza katika kikao hicho Kamishina Mwandumbya amesema uwamuzi wa kufunga biashara sio jambo la busara kwani licha ya kuwaathiri wafanyabiashara wenyewe pia madhara kama hayo uikumba na serikali ambapo sehemu kubwa ya mapato yake utokana na kodi zinazolipwa na wao.Read More

Share.

Comments are closed.