Monday, August 26

Serikali kufanya uhakiki wa Mashamba yote

0


Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imesema itafanya uhakiki wa mashamba yote yaliyopo Kilosa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kubaini yale yasiyoendelezwa ili yapendekezwe kufutwa kwa Rais.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu uamuzi wa kuyafuta mashamba 15 likiwamo la Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ufanywe Agosti 2017.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na  Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alibainisha hayo wakati akizungumza na wananchi wa Mvumi wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro, alipokwenda kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.

Alisema uamuzi wa Wizara yake kuamua kufanya uhakiki wa mashamba yote yaliyopo katika wilaya hiyo, unatokana na kubaini kuwepo dalili za upendeleo wakati wa kupendekeza mashamba 15 yaliyofutwa na Rais.

Kwa mujibu wa Lukuvi, Wilaya ya Kilosa ina jumla ya mashamba 183 na yote yatafanyiwa uhakiki na timu ya wataalamu 15 kutoka wizarani kwa lengo la kubaini mashamba yasiyoendelezwa na kuwasilisha mapendekezo kwake kwa lengo la kuyatolea uamuzi.


Share.

Leave A Reply