Tuesday, August 20

Kizazi cha baadae cha kumbukwa Bungeni

0


Mbunge wa Chambani, Yussuf Salim Hussein (CUF) ameiomba Serikali iongezee  fedha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ili iweze kupanga mipango ya ardhi kwa ajili ya kizazi cha baadae

Hussein ametoa kauli hiyo leo Mei 31, bungeni wakati akichangia Mjadala wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2019-2020.

“Wizara ya ardhi ndio inayobeba maisha yetu,Wizara hii inajukumu kubwa sana,ardhi haiongezeki lakini idadi ya Watanzania na mifugo inaongezeka mahitaji ya vitu vilivyopo juu ya ardhi inaongezeka lazima tuishauri ili tuwe na kilimo cha kisasa.

“Tujenge picha ya miaka 50 ijayo ambayo Watanzania wanaweza kufikia idadi ya watu milioni 100 itakuwaje, lazima Wizara iwezeshwe kupewa fedha ili ipange mipango ya ardhi.

“Tukiangalia miaka mitano au kumi tutaiachia matatizo makubwa kizazi chetu.Tuiombe Wizara itoe fedha nasema haya  ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhan vinginevyo tutajikuta katika hasara kubwa,”alisema Mbunge huyo.


Share.

Leave A Reply