Monday, August 26

Jibu la Serikali kwa waliojenga nyumba bondeni

0


Bunge limeelezwa kuwa serikali hairuhusu na haitavunja makazi ya watu waliojenga maeneo hatarishi ikiwamo mabondeni.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalumu,  Zainab Amiri (CUF).

Katika swali lake, mbunge huyo alisema kuna baadhi ya watu wanajenga kwenye mabonde, wengine jirani na hifadhi ya barabara na reli lakini serikali hukusanya kodi za maeneo na majengo katika maeneo hayo.

“Je, serikali inaeleza nini kuhusu kadhia hii, ili mwananchi ajenge mahali husika lazima apate kibali, je, nini adhabu ambayo wanapewa wanaotoa vibali kwenye maeneo hatarishi,” alihoji.

Akijibu swali hilo, Waziri Lukuvi amesema utoaji wa leseni za makazi hautafanyika kwa watu waliojenga maeneo hatarishi.

“Ni kweli kuna watu wanajenga kwenye hifadhi za barabara na hifadhi za miundombinu mingine na mabondeni lakini wamefanya hivyo kinyume na sheria, serikali hairuhusu na hata zoezi la urasimishaji na utoaji wa leseni za makazi,” amesema Lukuvi.


Share.

Leave A Reply