Thursday, August 22

YANGA KUCHEZESHWA NA WAAMUZI KUTOKA BURUNDI

0Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa kati ya Yanga ya Tanzania na Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6,2018 kwenye Uwanja wa Taifa saa 10.30 jioni.

Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya

Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17,2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.

Mwamuzi wa kati kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait Abou ,mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka Africa Kusini Gay Makoena.

*SIMBA YAPANGIWA WAAMUZI WA AFRICA KUSINI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) imewapanga waamuzi kutoka nchini Africa Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Africa Simba ya Tanzania itakapocheza na El Masry ya Misri Machi 7,2018 Uwanja wa Taifa saa 10 kamili jioni.

Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka Eritrea.

Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea .

Mwamuzi wa kati kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal Salem Embaia.

*CAF YATAJA WATANZANI SITA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO

Waamuzi wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Fosa Juniors ya Madagascar na As Port Louis ya Mauritius utakaochezwa Machi 18,2018 Madagascar.

Waamuzi walioteuliwa ni mwamuzi wa kati kati Elly Ally Sassii atakayesaidiana na Ferdinand Chacha mwamuzi msaidizi namba moja na Alli Kinduli mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Alphonce Mwandembwa na kamishna wa mchezo huo anatoka Seychelles, Lewis Blaze Madeleine

Wakati huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Msafiri Mgoyi ameteuliwa kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club Desportivo Costa Do Sol ya Msumbuji na Cape Town City ya Africa Kusini utakaochezwa Machi 7, 2018 Estadio Nacional Dol Zimpeto,Maputo

Naye Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameteuliwa kusimamia mchezo wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Zesco ya Zambia na Asec Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa Machi 7,2018 Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola.

Read More

Share.

Comments are closed.