Friday, August 23

WAZIRI MHAGAMA AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFUATA SHERIA ZA NCHI

0


 Waziri wa Nchi Ofisi, (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama wakati akitoa ufafanuzi jambo katika kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichojadili taarifa ya Utekelezaji wa bajeti 2017/2018 na makadirio ya bajeti ya mwaka 2018/2019 ya mafungu ya taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo Ofisi ya Msajii wa Vyama vya Siasa nchini, Leo Machi 28, 2018 katika ukumbi wa Mikutano Bungeni Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria , Mhe Najma Jiga akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichojadili taarifa ya Utekelezaji wa bajeti 2017/2018 na makadirio ya bajeti ya mwaka 2018/2019 ya mafungu ya taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo Ofisi ya Msajii wa Vyama vya Siasa nchini, Leo Machi 28, 2018 katika ukumbi wa Mikutano Bungeni Dodoma.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria , Mhe. Asha Abdallah Juma  akichangia hoja .
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria , Mhe. Saed Kubenea  akichangia hoja.
 Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Mhe Jaji Francis Mutungi wakiteta jambo   na Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe Antony Mavunde
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakiendelea na kikao
*****************************************************************

Vyama vya siasa nchini vimetakiwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa katika kudai haki katika masuala mbalimbali nchini ili kujiondoa katika matatizo yanayoweza kujitokeza na kuhatarisha amani ya nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi, (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama wakati akitoa ufafanuzi juu ya hoja za wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ziliyojitokeza wakati wa kujadili taarifa ya Utekelezaji wa bajeti 2017/2018 na makadirio ya bajeti ya mwaka 2018/2019 ya  mafungu ya taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo Ofisi ya Msajii wa Vyama vya Siasa nchini, Leo Machi 28,2018 katika ukumbi wa Mikutano Bungeni Dodoma.

“Kila raia anatakiwa kufuata na kutekeleza matakwa ya sheria  na taratibu zilizowekwa na nchi ili kujiondoa katika matatizo ambayo yanayoweza kujitokeza kutokana na ukiukwaji wa sheria, tujenge tabia ya utii wa sheria bila shuruti” amesisitiza Mhe Mgahama

Wakati wa majadiliano ilibainika kuwa vipo baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vimeonesha wazi kabisa kuvilazimisha vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za kisheria na kisha vyama hivyo hurudi kuilaumu Serikali.

Aidha, Mhagama amefafanua kuwa hoja zilizohusisha mgogoro wa ruzuku na uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), maandamano, migogoro ya vyama vya siasa na hoja zote ambazo kuna kesi makahamani, kuachwa bila kujadiliwa kwa kuwa kuzijadili hoja hizo kunaweza kuharibu mwenendo wa kesi na kushauri kuviachia vyombo husika kuendelea na taratibu zao kisheria.

Mhe. Mhagama ametoa wito kwa vyama vyote nchini kufuata utaratibu wa mahakama  wa kukata rufaa endapo vitaona haki haijatendeka .

Ikumbukwe siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeshindwa kufuata sheria na taratibu za nchi na kupelekea vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani, kitendo ambacho kimepelekea matendo ya uvunjifu wa amani

Kwa kutambua umuhimu wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, mmoja wa wajumbe wa kamati ya Katiba  na Sheria , Mhe Asha Abdallah Juma amempongeza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe Jaji Francis Mutungi kwa kazi nzuri anayoifanya ya kusimamia vyama vya siasa. Jambo liliungwa mkono na Mhe. Mhagama ambaye alisema kazi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inastahili pongezi na kutiwa moyo maana si kazi nyepesi.

Read More

Share.

Comments are closed.