Saturday, August 17

PAPII KOCHA ARUDI KUWASHIKA AANZA NA WAAMBIE, MSIKILIZE HAPA

0
Na Amina Kasheba, Dar
MWANAMUZIKI Papii Kocha hatimaye ameanza kuachia madini yake aliyokusanya kwa kipindi cha miaka 13 iliyopita akiwa jela kwa kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Waambie. 
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Papii Kocha amesema kuwa amenza na kibao hicho chenye ujumbe kwa wanadamu ili kuikumbusha Jamii kutokata tamaa katika maisha ilimradi tu wamejaaliwa pumzi.
Aidha amesema kuwa lengo la kuanza na wimbo huo ni kuwafanya watu wamkumbuke mungu kwa lolote wanalofanya hapa duniani na pindi wanapopatwa na majaribu ama mitihani ya kidunia katika harakati za maisha wasikate tamaa kwamwe. 
‘’Inabidi waamini kuwa kila jambo hupangwa na mungu na kwa malengo na makusudi yake ambayo sisi wanadamu hatuwezi kujua ya kesho ni yapi baada ya kupatwa na maswahibu’’ alisema Papii
Papii alisema kuwa japo kwa sasa kuna ushindani mkubwa katika soko la muziki lakini anaamini atafanya vizuri ili kuendana na soko hilo ambalo kwa sasa linazidi kuchechemea na kuwaachi njia vijana wa Bongo Flava watambe.

  “Nimerudi kufanya kazi tena ili kurudisha adhi ya muziki wa dansi kama ilivyokuwa kama enzi za wimbo wangu wa Seya, naamini mashabiki zangu na watanzania kwa ujumla watanipokea ili niweze kuusongesha muziki wa dansi kama nilivyopanga. Alisema PapiiRead More

Share.

Comments are closed.