Sunday, August 18

NGORONGORO HEROES YAWADUWAZA WAMOROCO

0


TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes, imeibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Bao hilo pekee katika mchezo huo la Ngorongoro Heroes, lilifungwa na Muksin Makame katika dakika ya 73 kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Morocco, Limourt Youssef kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Katika mchezo huo timu hizo zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu, huku zikitoa burudani safi kwa watazamaji walioingia bure uwanjani.
Baada ya mchezo huo, Ngorongoro Heroes Jumatano watacheza dhidi ya Msumbiji katika mchezo mwingine wa kirafiki kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Read More

Share.

Comments are closed.