Saturday, August 17

MWANAMITINDO NOEL ARUDI KIVINGINE, AJIVUNIA KUMVISHA LADY JAY DEE

0


Na Mwanaheri Masoud,Dar

BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu sasa Mwanamitindo Noel Ngale ameibuka na kuanza promosheni ya kazi zake mpya ambapo sasa ameanza kuzitangaza, akidai kuwa kimya kingi kina mshindo mkuu.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Noel, alisema kuwa Sanaa ya ubunifu ilimuingia damuni tangu akiwa shuleni na kupata hamu ya siku moja kuwa ni miongoni mwa wabunifu wanaowavisha watu maarufu duniani.

“Kiukweli Sanaa ya ubunifu ni kitu ambacho nilianza nikiwa shuleni, na nilikuwa na ndoto na shahuku ya kufika mbali zaidi na kutawaliwa na mawazo ya siku moja kuwavisha watu maarufu duniani,”alisema Noel.

Aidha alisema kwa sasa anashukuru mungu kwa hatua aliyofikia ya kuwavisha baadhi ya wasanii wakubwa hapa nchimi akiwemo Judith Wambura (Lady Jaydee)na wengine wengi .

Aliongeza kuwa kwa miaka mingi alitamani kuona ndoto yake ikitimia na kuwaajili vijana ili kuwaepusha na makundi mabaya .

Read More

Share.

Comments are closed.