Saturday, August 17

MTUNZI WA WIMBO WA "TANZANIA YETU NI NCHI YA KUPENDEZA" AMELAZWA ANAHITAJI MSAADA WA MATIBABU

0


Na Yusuph Mussa

Mzee Stephen Hizza (PICHANI), mtunzi na mwimbaji wa wimbo wa TANZANIA YETU NI NCHI YA KUPENDEZA, ambao aliutunga na kuimba mwaka 1966 akiwa na bendi ya Atomic Jazz ya mkoani Tanga, wakati Taifa letu linafikisha miaka mitano tangu tupate Uhuru mwaka 1961, amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wodi ya Kibasila namba 14 akiwa anaumwa Tezi Dume. 


Hakika mzee huyu ni moja ya HAZINA yetu kutokana na utunzi wa wimbo huo ambao unahamasisha uzalendo na kuipenda nchi yetu. 

Ombi kwa Watanzania, mwenye chochote ambacho anadhani kitamsaidia kupata afueni, basi amsaidie kwa kutumia namba hii 0657-513067.

Read More

Share.

Comments are closed.