Friday, August 23

MBOWE NA WENZAKE WASOMEWA DHAMANA BILA KUFIKA MAHAKAMANI

0


Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine watano wa chama hicho wameshindwa kufika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kwa ajili ya kusikiliza dhamana yao kwa sababu gari walilokuwa wamepanda kuharibika.

Hayo yameelezwa na Ofisa wa Magereza Inspekta Shaban ambapo amesema kuwa “Mbowe na wenzake wameshindwa kufika Mahakamani hapo kusomewa uamuzi wao kuhusu dhamana kwa sababu gari walilopanda limearibika”.

Aidha Inspekta huyo amethibitisha kuwa hakuna mtuhumiwa hata mmoja kutoka gereza la Segerea aliyefikishwa mahakamani hapo leo hii.

Baada ya kauli hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri amesema anatoa uamuzi kuhusu dhamana ya Mbowe na wenzake hata kama hawajafikishwa Mahakamani.

Viongozi hao wamepewa dhamana na mahakama hiyo kwa masharti ya kuwa na wadhamini 2 kila mshtakiwa atakayesaini Bondi ya Shilingi Milioni 20.
Hata hivyo Viongozi hao wametakiwa baada ya kutimiza masharti hayo wawe wanaripoti kituo cha polisi kila Alhamisi.

Mbowe pamoja na Viongozi wengine watano wa Chama hicho akiwepo Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Vicent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa pamoja na Mbunge wa Tarime Mjini Bi. Esther Matiko walifutiwa dhamana Machi 27 na kupelekwa mahabushu ya Segerea.Read More

Share.

Comments are closed.