Thursday, February 21

KMC YAAMUA KUACHANA NA HUMUDI, YAMTUPIA VILAGO RASMI

0


Uongozi wa Klabu ya Kinondoni municipal council (KMC) yaamua kumtupia rasmi vilago mchezaji wake Abdulhalim Humud baada ya leo kutangaza msimamo wao wa kumtimua mchezaji huyo aliyekithiri kwa utovu wa nidhamu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Katibu Msaidizi wa timu hiyo, Walter Harrison amesema mchezaji huyo amefukuzwa rasmi kutokana na utovu wa nidhamu kwa viongozi wake pamoja na wachezaji wenzake.

Harrison ameeleza kuwa, vitendo vya Humud vya utovu wa nidhamu vimekua vikijirudia mara kwa mara na uongozi kushindwa kuvikabili na kulazimika kumfukuza rasmi.

“Vitendo vya utovu wa nidhamu vimekuwa vikijirudia mara kwa mara, kwa viongozi na hata wachezaji wenzake na imepelekea kushindwa kuvumulia na kulazimika kuachana nae rasmi,”amesema Harrison

Aidha Humud alishawahi kuandika barua kwa uongozi wa KMC kuomba kuachwa ili asiendelee kuichezea timu hiyo kwa sasa na hivyo uongozi wakaamua alipe gharama kiasi kutokana na pesa nyingi zilizotumika kama vile gharama za matibabu, mshahara pamoja na fedha zilizokua zikitumika wakati akiwa kambini.

Kaimu Katibu huyo amekumbusha wadau na wanamichezo kuwa tabia hiyo kwa Humud imekua kama ni desturi yake kwani alishawahi kufanya vitendo hivyo kwa baadhi ya timu kongwe hapa nchini.

Share.

Leave A Reply