Monday, July 22

KINGWENDU 'FEKI' ALIVYOFUNIKA TAMASHA LA SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR

0


 UKIMUONA huwezi kuwa na mashaka kwamba huyu si Kingwendu halisi kuanzia muonekano, Sauti na mikogo yote ya Msanii wa vichekesho maarufu Kingwendu Ngwendulile Mzaramo wa Msanga Mkoa wa Pwani, lakini huyu ni Kingwendu wa Zanzibar, mzaliwa wa Kikwajuni aliyejitambulisha kwa jina la Arafati Hashim Kimwaga.

Msanii huyu ni aliibukia katika Tamasha la Biashara la kusherehekea Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, lililofanyika usiku wa jana (juzi) katika Viwanja vya Maisala mjini Zanzibar.

Katika Tamsha hilo baada tu ya mtangazaji kutangaza kupanda kwa msanii huyo uwanja mzima ulilipuka kwa shangwe huku wasiomjua wakihisi ni Kingwendu halisi kutokana na Sauti waliyokuwa wakiisikia, muonekano wake pamoja na miondoko akionekanakukopi kila anachopenda kufanya Kingwendu halisi.

Akizungumza na Uhuru baada ya onesho lake jukwaani hapo Kingwendu huyo wa Zanzibar, alisema kuwa muonekano wake umetokana na kumfuatilia kwa ukaribu msanii Kingwendu anayemkubari katika sanaa ya vichekesho kuliko msani mwingine yeyote ambapo ilimchukua muda mrefu kuweza kukopi na kujiweka kama Kingwendu hali kwa kila kitu hadi ndevu.

Aidha alisema kuwa ameweza kujizolea mashabiki lukuki mjini humo kutokana na kumudu kumuigiza ‘pacha’ wake Kingwendu na kuweza kusafiria nyota yake ipasavyo kwa kujipatia riziki ya watoto na mambo mengine na kuwashukuru waandaaji wa matamasha ambao wamekuwa wakimuunga mkono kila inapotokea Tamasha mjini humo.

”Kwa kweli namkubali sana Pacha wangu kingwendu kuliko msanii yeyote wa sanaa ya Vichekesho kutokana na yeye mwenye kujikubali na kujiamini kiasi cha kuthubutu kujitosa kwenye kinya’anyiro cha kuwania Ubunge msimu uliopita, lakini hata mimi mjini hapa nashukuru wananchi wananikubali na kunishukuru kwa kumuwakilisha vyema,

Ikitokea siku amealikwa katika Tamasha fulani hapa kwetu na akawa na shughuli nyingi kiasi cha kushindwa kufuja basi asisite aniambie tu mimi ntamuwakilisha na hakuna atakayehisi kuwa si Kingwendu halisi, alisema Kingwendu feki.

 Msanii wa Vichekesho Arafati Hashimu Kimwaga ‘Kingwendu wa Zanzibar’ akishambulia jukwaa na shabiki wake Asma Mustafa, wakati wa Tamsha maalumu la Biashara kusherehekea miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar, lililofanyika katika Viwanja vya Maisala mjini Unguja.

Share.

Leave A Reply