Saturday, July 20

Waziti Kangi Lugola: Mashoga wapo salama nchini, anaetishwa aende Polisi

0


Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kangi Lugola amesema kuwa wapenzi wa jinsia moja hawapo hatarini nchini humo.

Lugola amesema japo ushoga ni kosa la jinai nchini Tanzania, wanaojihusha na vitendo hivyo hawatishiwi maisha na wala hawaikimbii nchi.

Akizungumza na gazeti la serikali la Habari Leo, Lugola amekanusha kuwa wapenzi wa jinsia moja wapo hatarini.

“Ninachosema ni kuwa Tanzania ni salama na hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kuwa sio salama bila ya kuwa na vigezo husika, kama mtu yeyote anahatarishiwa maisha yake, basi anapaswa kwenda Polisi na mimi sijapata taarifa zozote kutokea Polisi zinazoelezea kuwapo kwa mazingira hatarishi ya watu hao,” alisema.

Alisisitiza kuwa kwa upande wa mashoga, hajapata taarifa kutoka kituo chochote cha Polisi nchini, wakilalamikia usalama wao.

Alisema kama kungekuwa na mazingira sio salama kwao, wangeenda kupeleka malalamiko yao kwenye vituo vya Polisi jirani; na kuwa akiwa waziri mwenye dhamana, hajapata taarifa za mazingira hatarishi kwa mashoga nchini.

Hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwataka wananchi kumtajia majina ya mashoga wa Dar es Salaam, kwa njia ya simu yake ya mkononi. 

Kutokana na agizo hilo, watu kadhaa wamekuwa wakiendelea kumtajia majina hayo, hali ambayo imesababisha taharuki kwa baadhi ya watu waliotajwa, huku wengine wakilalamikia utaratibu huo, hasa mashirika ya haki za binadamu yakiwamo ya nje ya nchi.

DOWNLOAD APP YETU YA MASAMA BLOG HAPA👇👇👇ILI UWE UNAPATA HABARI HIZI KIRAHISI

Share.

Leave A Reply