Monday, August 19

WAZIRI NDALICHAKO AFANYA UKAGUZI WA HATUA ZA MAANDALIZI YA UWEKAJI JIWE LA MSINGI JENGO LA CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA MBEYA

0


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea na kukagua hatua za maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya, ambapo amepongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua za ujenzi ulipofikia.

Akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Kusiluka, Prof Ndalichako amemwelekeza Mkandarasi wa Ujenzi kuhakikisha kufikia Juni 2019 ujenzi wa Jengo hilo kuwa umekamilika kama ilivyopangwa.

Kukamilika kwa ujenzi kutawezesha jumla ya wanafunzi 900 kupata vyumba vya madarasa mbali na kumbi za mikutano na ofisi za uendeshaji. Jengo hilo linatarajiwa kuwekwa jiwe la Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli Mei 1, 2019.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (katikati) akikagua mahali litakapojengwa jiwe la msingi ambalo litawekwa rasmi na Rais wa Jamhuri wa Muuungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Mei 1, 2019. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka na kulia ni Mkadarasi wa Ujenzi Injinia Thedeus Koyanga (mwenye shati la mikono mirefu) akifuatiwa na Profesa Ernest Kihanga Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.

Waziri Ndalichako akiongozwa na Mkandarasi wa mradi akikagua vyuma vya madarasa mara alipowasili kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa tano la Taaluma na Utawala linalotazamiwa kumalizika mwezi Juni,2019. Pamoja naye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka, Naibu Mawakamu Mkuu wa Chuo Utawala na fedha Prof. Ernest Kihanga na wasimamizi wa ujenzi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiweka saini kwenye kitabu cha wageni kwenye eneo la ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya mbeya mara tu baada ya kuwasili. Aliyeshika kitabu ni Injiani Thadeus Koyanga na kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka ( Mwenye Kaunda suti kushoto).

Profesa Joyce Ndalichako alikagua muonekano wa nje wa jengo la Taaluma na Utawala la chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya pamoja na kukagua usafi wa mazingira, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi kabla Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli hajafika kuweka jiwe la msingi.

from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2UWtB2C
via

logoblog

Thanks for reading WAZIRI NDALICHAKO AFANYA UKAGUZI WA HATUA ZA MAANDALIZI YA UWEKAJI JIWE LA MSINGI JENGO LA CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA MBEYA

Share.

Leave A Reply